NAPENDA SANA SEX” - G NAKO
Imeandikwa na: Irene Robinson na Abdul
Mbwambo.
Sio kitu cha kushangaza tena ukikuta msichana
ananyanyua simu na kumpigia kijana kumtaka kimapenzi. Wala haishangazi kukuta
kijana ana wapenzi zaidi ya mmoja na pengine wote wanajuana kwenye mzunguko
huo. Wala sio “surprise” tena kukuta vijana wamekaa kistoni, wakizungumza na
kuchambua aina za mahusiano waliyonayo, kuanzia yale ya mbio fupi, mchepuko,
friends with benefits na wakati mwingine mwenye wengi ndio kinara.
Ndio maana msanii G-Nako kutoka weusi na yeye
alipoulizwa na DJ Tee, mtangazaji wa kipindi cha Shujaaz Radio Show kuhusu ni
kundi gani kati ya vijana wa kike na kiume ambalo hufikiria sex zaidi katika
michakato yao ya kila siku, aliamua kufungua roho kuhusu hili. Huku
akijifikiria kwa umakini, G-Nako alisema hawezi kusema kwa uhakika kwamba ni
jinsia gani inapenda sex zaidi ya nyingine. “It depends na mtu na mtu, kwa
mfano kama mimi hapa napenda sex sana” alisema mkali huyu wa Go Low.
Katika mjadala mkali wenye mihemko ya kutosha
uliofanywa na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wa kundi la Madada Sita wakiwa
na vijana wengine, wasichana walisikika wakiwatuhumu wavulana kwa kupenda sex
zaidi ya wanawake na wavulana wakijaribu kutoa kila sababu za kuonesha kwamba
wasichana ndio wanaendekeza zaidi kamchezo hako. Msanii Lizzy wa kundi hilo
lenye maskani yake TMK, alisema kwamba ingawa msichana anaweza kuwa na wanaume
zaidi ya mmoja haimaanishi anakusudia kufanya nao mapenzi wote. Alitolea mfano
kwamba msichana anaweza kuwa na bwana kwa ajili ya mavazi, mwingine kwa
chakula, na mwingine kwa kumnunulia vifaa vya urembo na mwingine kwa ajili ya
kufanya nae mapenzi tu. “Ikitokea mwanaume anaanza kuniambia tufanye sex na
akiendelea kusisitiza nitamuacha” Alisema mmoja wa wasanii hao wa Madada Sita
Akijaribu kuwatetea wanaume katika mjadala huo,
Walter ambaye ni mmoja kati ya Managers wasaidizi wa kundi hili linalokuja kwa
kasi na ngoma yao ya “Matobo” alisema kwamba wanawake ndio hupenda kufikiria
sex zaidi kwa kuwa hata mtaani wanawake ndio hujiuza zaidi ya wanaume. Kauli
hii ya Walter ilifanya ashambuliwe kwa maneno na akina dada hao huku wakisema
kwamba siku hizi kuna wanaume wengi tu ambao wanajiuza pia na wanajulikana kwa
jina maarufu kama Marioo, hivyo sio akina dada pekee yao wanaobadilisha ngono
kwa pesa.
Mtaalamu wa afya kutoka katika chuo kikuu cha Dar
es salaam Dr. Tuholani alitoa ufahamu wake kwa kusema kwamba suala la kupenda
kufanya sex ni jambo la kisaikolojia na linaweza kuwa pande zote. “nilikuwa na
rafiki yangu wakati tukiwa shule akasema hakuwa anapenda kufanya mapenzi na
mwanaume kwa sababu aliwahi kubakwa akiwa na miaka 11, jambo lililomuharibu
kisaikolojia na kuwachukia wanaume” alisema Dr Tuholani akizungumzia majibu
aliyopewa na rafiki yake huyo. Hata hivyo DR. Tuholani alisema kuwa wanawake
mara nyingi huwa na vipaumbele vingi vinavyoweza kuwafanya wasifikirie mapenzi
tofauti na ilivyo kwa wanaume.
Tafiti zilizochapishwa na mitandao wa ell/msnbc.com
zinasema asilimia 66 ya wanaume walioko kwenye mahusiano wanapata hamu ya
kufanya mapenzi tofauti na asilimia 25 ambayo ni wanawake.
Sex ni moja kati ya basic needs katika maisha ya
wanadamu na baadhi ya viumbe, japokuwa hutegemea na hali ya mazingira
yanayoweza kusukuma hamu ya kuhitaji au kutohitaji tendo hilo. Je wewe
unaonaje? Wanawake ndio huendekeza Sex zaidi ya wanaume?
Comments
Post a Comment